news
News

Good morning -Kidfarmaco primary Kerra Road Commissioning

Tarehe 8/7/2019, tulijumuika pamoja na wakaazi wa Kidfarmaco Kikuyu ward kwa uzinduzi wa ukarabati wa barabara ya good morning -Kidfarmaco primary chini ya kamati ya CRC-Kerra.

Tulipata nafasi pia ya kulikabidhi kundi la kina mama la kid Garden viti hamsini zitakazo wasaidia kujiinua kiuchumi kwa kuongeza mapato kwa kundi lao.

Baadaye tuliweza kukagua mradi unaoendelea chini ya hazina ya NG-CDF wa ujenzi wa jengo la afisi za Shule ya msingi ya Thogoto Primary. 
Hapo jioni tukajiunga na wakazi wa Ndiguini kuendeleza ukarabati wa barabara ya ndiguini primary na pia kukabidhi rasmi darasa la kwanza kabisa la shule mpya ya msingi ya Ndiguini.

Tunajiandaa kwa ujenzi wa madarasa mengine mawili kabla ya mwisho wa mwaka huu chini ya hazina ya NG-CDF-Kikuyu.

 

 

 

 

 

Downloadable Files

No files available yet

0 Comment s So Far

There are no comments yet.

Authentication required

You must log in to post a comment.

Log in